Date: 
10-08-2023
Reading: 
1Yohana 1:5-7

Alhamisi asubuhi tarehe 10.08.2023

1 Yohana 1:5-7

5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.

6 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Tuenende kwa hekima;

Yohana anaandika kwamba Mungu ni nuru, hamna giza ndani yake. Kusema kwamba tunamfuata Kristo wakati hatutendi yaliyo mapenzi yake ni uongo, maana yeye yuko nuruni na siyo gizani. Tukienda nuruni tunasafishwa dhambi zetu, maana Mungu hapendi tukae gizani.

Yohana aliandika maneno haya kama utangulizi, kisha akasisitiza ungamo la dhambi;

1 Yohana 1:8-9

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.

9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

Kumbe tukitubu dhambi zetu tunasamehewa. Tunatoka gizani na kuingia nuruni. Hekima ya Mungu ituongoze kuishi maisha ya toba ili kukaa nuruni na kuurithi uzima wa milele. Amina.

Alhamisi njema.

 

Heri Buberwa