Date: 
08-08-2023
Reading: 
2 Wakorintho 3:1-3

Jumanne asubuhi tarehe 08.08.2023

2 Wakorintho 3:1-3

1 Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu?

2 Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;

3 mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

Tuenende kwa hekima;

Mtume Paulo anawaambia waamini wa Kanisa la Korintho kwamba kujisifu hakufai mbele za Mungu. Anawaambia kuwa maisha yao yanaweza kuwa barua, yaani ushuhuda unaomhubiri Kristo. Msingi wa Paulo katika maisha ya imani uko katika matendo ya waaminio kuwa barua kwa wengine, na siyo kujisifu na kujitangaza mbele za watu.

Wito unatujia asubuhi hii, kwamba tusiishi kwa kujisifu, na kuwa wakristo kusitufanye kutosheka na kuridhika, bali matendo yetu yamuakisi Kristo. Maisha yetu yawe ushuhuda kwa wengine yakimpa Mungu Utukufu. Tunakuwa na maisha yenye ushuhuda tukienenda kwa hekima ya Mungu. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa