Date: 
26-07-2023
Reading: 
Luka 10:38-42

Jumatano asubuhi tarehe 26.07.2023

Luka 10:38-42

38 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.

39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.

40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.

41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;

42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Uchaguzi wa busara

Yesu aliingia nyumbani kwa Martha ambaye alikuwa na ndugu yake aitwaye Mariamu. Wakati Martha akiendelea na maandalizi ya kumkaribisha mgeni pale nyumbani, Mariamu yeye alikaa akimsikiliza Yesu. Martha aliona Mariamu hamsaidii, maana badala ya kusaidia kuandalia mgeni yeye alikaa tu kumsikiliza Yesu. Lakini bado Yesu alisema Mariamu alichagua fungu jema kumsikiliza Yesu.

Mazingira hayawekwi wazi zaidi, lakini najaribu kuwaza; kwamba Mariamu aliamua kukaa na Yesu kwa sababu alimuona yuko mwenyewe, au alikuwa na hamu ya kumsikiliza Yesu, maana huenda hakuwahi kupata fursa kama hiyo n.k

Vyovyote iwavyo, Martha aliyemkaribisha Yesu alichagua kwa busara, na Mariamu aliyekaa kumsikiliza Yesu alichagua kwa busara. Uchaguzi wa busara mkubwa kuliko vyote ni kumchagua Yesu maishani. Siku njema 

 

Heri Buberwa 

Mlutheri