Date: 
26-05-2023
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 26:7-9

Ijumaa asubuhi tarehe 26.05.2023

Kumbukumbu la Torati 26:7-9

7 Tukamlilia Bwana, Mungu wa baba zetu; Bwana akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu.

8 Bwana akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu;

9 naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali.

Usikie kuomba kwetu;

Mungu aliwaahidi Israeli kuiendea nchi ya ahadi, na aliwaelekeza wakifika huko kumtolea sadaka ya shukrani kwa ajili ya kuwakomboa kutoka utumwani. Somo la asubuhi ya leo, ni sala ambayo Israeli wanaelekezwa kusali baada ya kufika kwenye nchi ya ahadi. Wanamshukuru Mungu kwa kuwatoa Misri na kuwaingiza katika nchi ijaayo maziwa na asali.

Israeli walielekezwa kumshukuru Mungu kwa sababu ya kuwakomboa toka utumwani. Sisi leo tunawajibika kumshukuru Mungu kwa kutuokoa na kutufanya watoto wake. Yeye hutushindia katika mambo yote na kutupa mafanikio. Tunaalikwa kudumu katika Bwana tukiomba na kumshukuru Mungu maana yeye husikia kuomba kwetu.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa