Date: 
16-03-2022
Reading: 
Mathayo 2:16-18

Hii ni Kwaresma tarehe Jumatano asubuhi 

16.03.2022

Mathayo 2:16-18

16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,

18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

Tupinge ukatili;

Kanisa la kwanza liliwatambua watoto waliouawa kwa amri ya Herode Mkuu wakati wa kuzaliwa kwa Yesu (inakadiriwa 7-2KK) kama mashahidi wa kwanza wafia imani, kwa sababu waliuawa bila hatia, Herode akiwa na wasiwasi na utawala wake.

Herode aliona suluhisho la uhakika wa utawala wake ni kuwaua watoto wadogo wote waliozaliwa, ili awe na uhakika wa kuwa amemuua Yesu, ambaye alisikia angekuwa mtawala wa Israeli. Herode aliona angefanikiwa kubaki madarakani kwa kuwaua wengine!

Inawezekana tupo baadhi yetu ambao tuko tayari kuangamiza wengine kwa maslahi yetu. Bado tupo wenye roho ya Herode? Roho ya uuaji, iliyo tayari kuua ili kujinufaisha? Huo ni ukatili, ni uovu, acha mara moja. Kristo anatualika kuacha roho mbaya, tukimtumikia kwa kuwapenda wengine kama yeye alivyotupenda sisi akatufia msalabani. Acha ukatili.

Uwe na siku njema.