MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 20 MACHI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA NI

TUTUNZE UUMBAJI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.

3. Matoleo ya Tarehe 13/03/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu, pamoja na Semina zinazoendelea kipindi chote cha Kwaresma siku ya Alhamisi na Ijumaa pamoja na Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Leo tarehe 20/03/2022 tumetembelewa na Wanafunzi wa Ukwata kutoka Sekondari ya Kisutu. Watashiriki ibada zote za leo. Karibuni sana.

6. Jumapili ijayo tarehe 27/03/2022 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

7. NYUMBA KWA NYUMBA

- Masaki na Oyserbay: Watashiriki ibada ya jumatano hapa Usharikani

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Lawrence Mlaki.

8. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Pili. Pamoja na kuhudumu ibada ya Jumatano.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.