MATANGAZO YA USHARIKA    

TAREHE 08 JANUARI, 2023        

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

UBATIZO WETU    

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 01/01/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Darasa la Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili litaanza jumamosi ijayo tarehe 14/01/2023 saa 3.00 asubuhi. Wazazi mnaombwa kuwahimiza watoto wasikose na wafike kwa wakati. Aidha Uongozi wa Usharika unaendelea kuwahimiza wazazi wenye watoto waliofikia umri wa kuanza mafundisho ya Kipaimara kuwaandikisha Mwaka wa I wachukue fomu ofisi ya Parish Worker.

5. Leo tarehe 08/01/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

6. Kila Msharika unatakiwa kujaza fomu ili kuhakiki namba kwa Mwaka 2023. Wazee watagawa fomu hizo. 

7. Ijumaa ijayo tarehe 13/01/2023 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Wazee. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria.

8. SHUKRANI - JUMAPILI TAREHE 15/01/2023

IBADA YA 3 SAA 4.30 ASUBUHI

  • Familia ya Dudley Gabriel Mawalla watamshukuru Mungu kwa kuwatia nguvu tangu kuondokewa na mke wake Patricia aliyetwaliwa na Bwana.

Neno: Zaburi 28:7, Wimbo: TMW 51 (YESU NDIYE KIONGOZI)

  • Familia ya Marehemu Mama Nsia Jonathan Kimaro watamshukuru Mungu kwa maisha ya mama yao Nsia Jonathan Mwanga Kimaro na kuwatia nguvu.

Neno: Zaburi 23, Wimbo: TMW 424 (NIONAPO AMANI)

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Felix Mosha Regent Estate Alhamisi saa 12 jioni

10. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 14/01/2023. AMBAYO ITAKUNGWA ST. JOSEPH UPANGA

Bw. Jackson Simon Shekigenda na Bi. Winfrida Zablon Kimaro

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza. 

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.