MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 18 MARCH, 2018
SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU NI MPATANISHI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Jumatano ijayo tarehe 21/03/2018 tunaendelea na ibada ya Kwaresma kama kawaida. Washarika wote mnahimizwa kuiadhimisha. Tunaendelea na mafundisho maalumu juu ya "MAMLAKA UWEZA NA NGUVU YA DAMU YA YESU". Mafundisho yatakuwa ni siku tatu kama kawaida Jumatano, Alhamis na Ijumaa kuanzia saa 11.00 jioni. Jumuia ya OYSTERBAY/MASAKI NA KIJITONYAMA/ SINZA/MWENGE/ MAKUMBUSHO/ UBUNGO itaongoza liturgia ya ibada ya Kwaresma siku ya Jumatano, Kwaya zitakazohudumu ni Kwaya Kinamama na Kwaya ya Tarumbeta. Aidha Maombi na Maombezi siku za Alhamisi yataendelea kwa kipindi cha Kwaresma, yakiambatana na mafundisho maalum.
4. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kwamba jumamosi ijayo tarehe 24/03/2018 saa 4.00 asubuhi tutakuwa na ibada maalum itakayoambatana na Chakula cha Bwana kwa washarika wetu wote wenye umri kuanzia miaka 65 na kuendelea. Pia kutakuwa na maongezi ya pamoja. Wazee wote hao wanakaribishwa.. Kwa Wazee ambao watahitaji huduma ya usafiri tunaomba taarifa zao kwenye ofisi ya Chaplain.
5. Uongozi wa Umoja wa Wanawake (UWA) unapenda kuwakumbusha wanawake kuwa maadhimisho ya pasaka Kijimbo ni jumamosi ijayo tarehe 24/03/2018 katika Usharika wa Ukonga kuanzia saa 2.00 asubuhi. Hivyo Wanawake wote muungane na Kwaya ya wamama kwa ajili ya maandalizi siku hiyo.
6. Jumapili ijayo tarehe 25/03/2018 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi familia ya Mzee Anold Kilewo watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea
Neno:Zaburi 121:1-3, Wimbo: TMW 430 (Tufani inapovuma) Kwaya ya Upendo
7. Mazoezi ya maandalizi ya Kantate yameshaanza kila siku ya Jumanne kuanzia saa 11.00 jioni. Wanakwaya wa Kwaya zote za mnaombwa kuhudhuria.
8. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: Watashiriki semina hapa usharikani
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkony
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watashiriki semina hapa usharikani
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watashiriki semina hapa usharikani
- Mjini kati: Kwa Mama Rwanshane
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Peter Mlagha
- Tabata: Kwa Bwana na Bibi Mwakasege
Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.