MATANGAZO YA USHARIKA

  TAREHE 15 JULAI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI NEEMA YA MUNGU YATUWEZESHA KUZAA MATUNDA MEMA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2 Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti.

3. Mungu ameendelea kujidhihirisha kila tunapokutana kwa masomo, maombi na maombezi. Hivyo Mwl. Mgisa Mtebe, katika ibada za asubuhi (Morning Glory) ataendelea na somo la UTAKASO KAMILI kesho siku ya jumatatu tarehe 16/07/2018 hadi ijumaa tarehe 20/07/2018.   Aidha siku ya alhamisi tarehe 19/07/2018 kuanzia saa 11.30 jioni tutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi.  Washarika wote mnakaribishwa. 

4. Mkutano wa Vicoba ya Wajane na Wagane wa Azania Front utafanyika jumamosi ya tarehe 28/07/2018 saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo.

5. Leo mara baada ya ibada ya pili kutakuwa na uchaguzi wa uongozi wa Umoja wa Vijana hapa usharikani. Vijana wote wanahimizwa kuwepo ili kufanikisha kupata viongozi wapya kwa muhula ujao.  Wajumbe wa kamati ya malezi wanaombwa kuwepo kusimamia zoezi hilo.

6. NDOA.

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 04/08/2018

SAA 06.00 MCHANA

Bw. Nacha Fredrick Mlaki         na     Bi Mbeyu Sia Issangu

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28/07/2018

NDOA HII ITAFUNGWA RUJEWA MBEYA

Bw. Bringtona Mangula         na     Bi Janeth Jackson Msuya

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 21/07/2018

SAA 08.00 MCHANA

Bw. Mika Mathayo Ndosa         na     Bi Marystela Kondo Benedict

SAA 09.00 ALASIRI

Bw. Amani Goodluck Kamnde     na     Bi Anna Cecilia Katarina Westman

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu

7. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Watatangaziana

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale

- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero

- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Victor Kida

- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi David Mollel

- Mjini kati:  Kwa Mama Omega Mongi

- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:Kwa Bi Mary Kinisa

- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Allen David

- Tabata: Watatangaziana

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.