MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 03 SEPTEMBA, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MATUMIZI YA ULIMI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
3. Leo hatutakuwa na kipindi cha Maombi na Maombezi hapa Usharikani ila kutakuwa na Tamasha la Vijana. Siku ya Alhamisi 07/09/2017 kutakuwa na kipindi cha Maombi na Maombezi kama kawaida. Wote mnakaribishwa.
4. Vitenge vya Kiharaka bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10. Kama umeshanunua unaweza kumnunulia ndugu, rafiki ili tuweze kufanikisha ujenzi wa kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.
5. Leo 03/09/2017 tutamtolea Mungu Fungu la kumi. Washarika karibuni.
6. Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii Azania Front inapenda kuwataarifu kuhusu mabadiliko ya tarehe ya Semina ya Elimu ya Afya kwa watoto wa Kipaimara 2017. Kutokana na sababu zisizozuilika semina hii sasa itafanyika tarehe 16/09/2017 badala ya tarehe ya awali 23/09/2017. Aidha kutokana na mabadiliko hayo Semina ya mwaka huu itawahusu watoto wa Kipaimara tu na wale waliohitimu hivi karibuni wenye umri hadi miaka 15. Semina iliyatarajiwa kufanyiwa wazazi wa watoto hawa itafanyika mwakani. Tunaomba samahani kwa usumbufu uliojitokeza na tuiombee sana siku hiyo.
7. Jumapili ijayo tarehe 09/09/2017 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisi ya Mchungaji.
8. Uongozi wa Umoja wa vijana unapenda kuwakaribisha wazazi, walezi, vijana na washarika kwa ujumla kwenye tamasha la maigizo litakalofanyika leo tarehe 03/09/2017 hapa Usharikani mara baada ya ibada ya pili saa 7.30 mchana. Kutakuwa na vikundi mbalimbali toka Sharika na Mitaa. Aidha Umoja wa Vijana Dayosisi ya Mashariki na Pwani unapenda kuwataarifu vijana wote kuwa katika kuadhimisha miaka 500 ya matengenezo ya kanisa, umeandaa mkesha maalum wa vijana unaoitwa USIKU WA KIJANA NA MATENGENEZO YA KANISA. Katika mkesha huo, vijana watafundishwa mada mbalimbali zinazohusu matengenezo ya Kanisa. Mkesha huo utafanyika katika Usharika wa Ubungo siku ya Ijumaa tarehe 08/09/2017 kuanzia saa 2.30 usiku mpaka saa 11.00 alfajiri. Vijana wote mnakaribishwa kushiriki tukio hili muhimu kwa historia ya Kanisa letu.
9. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaarifu wazazi wote kuwa, mwaka huu watoto watavaa Tshirt za miaka miatano ya matengenezo ya Kanisa katika sikukuu yao ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba wazazi muwanunulie watoto Tshirt hizo. Bei ya TShirt moja ni sh. 10,000/=. Wazazi mnaombwa kupeleka fedha hizo kwa mhasibu wa Usharika ili zikachukuliwe kwa pamoja.
10. NDOA
NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 23/09/2017
NDOA HII ITAFUNGA KANISA LA KATOLIKI ST. PETER
Bw. Paul Kennedy Ongoma na Bi. Shanga Prize Naomi Jackson Kaale
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/09/2017
SAA 08.00 MCHANA
Bw. Samson Felix mkwama na Bi. Naomi Joel Kiangi
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: Kwa Georgina Kisamo
- Kinondoni: Kwa Mama Tabu Ndziku
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Dk na Bibi D. Ruhago
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mama Stella Sykes
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Dallas Mwanauta
- Tabata: Watatangaziana
- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Mamkwe
- Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Wilfred Moshi
Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.