Event Date: 
17-11-2020

Kwaya ya wanawake ya Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront hivi karibuni ilitembelea kituo cha watoto yatima cha Kiwalani kilichopo jijini Dar es salaam kinachowatunza na kuwasomesha watoto yatima wapatao 50 wa jinsia zote katika ngazi ya elimu ya sekondari.

Kwaya ya wanawake ya Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront ikikabidhi msaada wa vyakula pamoja na fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendeshaji wa kituo cha kulea watoto yatima cha Kiwalani kilichopo jijini Dar es Salaam.

Waimbaji wa kwaya ya wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima cha Kiwalani jijini Dar es Salaam

Kwaya ya wanawake ya Usharika ilifanya ziara hiyo baada ya kupata mwaliko wa kwenda kutembelea kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mahafali ya watoto waliokuwa wanamaliza kidato cha nne.

Kwaya ya wanawake wakiimba walipozuru kituo cha kulea watoto yatima cha Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Kwaya ya wanawake ya Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront wakimtukuza Mungu kwa wimbo walipozuru kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani.

Mahafali hayo yalienda sambamba na kwaya kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao pamoja kufanya changizo ya kujenga bweni na darasa kwa ajili ya kituo hicho. Kwaya ya wanawake pia ilishiriki kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula kama mchele, unga, sukari pamoja na fedha taslim kwa ajili ya ujenzi wa bweni na darasa.

 

Habari na Picha vimekusanywa na Jane Mhina