Date: 
25-04-2017
Reading: 
Joshua 1:1-7 (NIV)

TUESDAY 25TH APRIL 2017 MORNING                          

Joshua 1:1-7 New International Version (NIV)

Joshua Installed as Leader

1 After the death of Moses the servant of the Lord, the Lord said to Joshua son of Nun, Moses’ aide: “Moses my servant is dead. Now then, you and all these people, get ready to cross the Jordan River into the land I am about to give to them—to the Israelites. I will give you every place where you set your foot, as I promised Moses. Your territory will extend from the desert to Lebanon, and from the great river, the Euphrates—all the Hittite country—to the Mediterranean Sea in the west.No one will be able to stand against you all the days of your life. As I was with Moses, so I will be with you; I will never leave you nor forsake you. Be strong and courageous, because you will lead these people to inherit the land I swore to their ancestors to give them.

“Be strong and very courageous. Be careful to obey all the law my servant Moses gave you; do not turn from it to the right or to the left, that you may be successful wherever you go.

God calls different people to fulfill His purposes. God called Moses, and when his works was finished, God called Joshua.

God equipped Joshua and gave him instructions and the promise of His presence.

Let us listen to God’s call and instructions to us and obey and trust Him always. 

JUMANNE TAREHE  25 APRILI ASUBUHI                                 

YOSHUA 1:1-7

1 Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, 
2 Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. 
3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. 
4 Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu. 
5 Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. 
6 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. 
7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. 
      

Mungu anawaita watu mbalimbali kila mtu kwa wakati wake na kwa nafasi yake. Mungu alimwita Musa kuongoza Waisraeli. Baada ya Musa alimwita Yoshua. Mungu alimpa Yoshua agizo na ushauri wa kufuata. Mungu aliahidi kuwa naye.

Mungu anatupa sisi kazi za kufanya. Tumsikilize Mungu na tumtii na tumtegemee siku zote za maisha yetu.