Date: 
22-03-2018
Reading: 
John 7:25-32 (Yohana 7:25-32)

THURSDAY 22ND MARCH 2018 MORNING                                  

John 7:25-32 New International Version (NIV)

Division Over Who Jesus Is

25 At that point some of the people of Jerusalem began to ask, “Isn’t this the man they are trying to kill? 26 Here he is, speaking publicly, and they are not saying a word to him. Have the authorities really concluded that he is the Messiah? 27 But we know where this man is from; when the Messiah comes, no one will know where he is from.”

28 Then Jesus, still teaching in the temple courts, cried out, “Yes, you know me, and you know where I am from. I am not here on my own authority, but he who sent me is true. You do not know him, 29 but I know him because I am from him and he sent me.”

30 At this they tried to seize him, but no one laid a hand on him, because his hour had not yet come. 31 Still, many in the crowd believed in him. They said, “When the Messiah comes, will he perform more signs than this man?”

32 The Pharisees heard the crowd whispering such things about him. Then the chief priests and the Pharisees sent temple guards to arrest him.

Jesus is debating with the people. They are wondering who He is. They think that He might be the Messiah but they are not sure. This made the Pharisees annoyed. They feel that Jesus is too popular. They are jealous of Him.

Even today people have many different ideas about Jesus Christ. Do you truly understand who He is?

Who is Jesus in your life? 

ALHAMISI TAREHE 22 MACHI 2018 ASUBUHI                         

YOHANA  7:25-32

25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? 
26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? 
27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. 
28 Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 
29 Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. 
30 Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. 
31 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? 
32 Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate. 

Watu walitafakari kuhusu Yesu Kristo. Walitaka kujua Yesu  ni nani. Yesu alijua wanawaza nini. Mafarisayo walisikia na walikasirika kusikia kwamba watu wanasema Labda ni Mesihi.

Hadi leo watu wana mawazo mbalimbali kuhusu Yesu.

Wewe Je! Unafikiri nini juu ya Yesu? Umempa Yesu Nafasi gani katika maisha yako?