Date: 
14-05-2022
Reading: 
Isaya 40:26-31

Jumamosi asubuhi tarehe 14.05.2022

Isaya 40:26-31

26 Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.

27 Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?

28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Israeli wanapewa ujumbe wa kumtazama Bwana aliye muumbaji, aliyeko mahali pote. Bwana ndiye huwa nguvu watu wake, na kuwapa nvuvu wasio na uwezo. Israeli wanaahidiwa nguvu mpya pale watakapodumu katika Bwana.

Tunapewa ujumbe wa kumtazama Bwana maishani mwetu. Ni ahadi idumuyo milele kuwa tutapokea nguvu za kushinda katika njia zetu tukimtegemea Bwana. Njooni tumrudie Bwana, ili tuwe na maisha mapya katika yeye.

Siku njema.