Date: 
19-04-2018
Reading: 
Isaiah 43:1-7 (Isaya 43:1-7)

THURSDAY  19TH APRIL 2018 MORNING                         

Isaiah 43:1-7 New International Version (NIV)

Israel’s Only Savior

But now, this is what the Lord says—
    he who created you, Jacob,
    he who formed you, Israel:
“Do not fear, for I have redeemed you;

    I have summoned you by name; you are mine.
When you pass through the waters,
    I will be with you;
and when you pass through the rivers,

    they will not sweep over you.
When you walk through the fire,

    you will not be burned;
    the flames will not set you ablaze.
For I am the Lord your God,
    the Holy One of Israel, your Savior;
I give Egypt for your ransom,

    Cush[a] and Seba in your stead.
Since you are precious and honored in my sight,
    and because I love you,
I will give people in exchange for you,

    nations in exchange for your life.
Do not be afraid, for I am with you;
    I will bring your children from the east
    and gather you from the west.
I will say to the north, ‘Give them up!’
    and to the south, ‘Do not hold them back.’
Bring my sons from afar

    and my daughters from the ends of the earth—
everyone who is called by my name,
    whom I created for my glory,
    whom I formed and made.”

Footnotes:

  1. Isaiah 43:3 That is, the upper Nile region

Speaking through the Prophet Isaiah God brings words of comfort to His people. The people were in exile because of their sins and rebellion against God. But now God promises to gather them together again and to care for them.

God loves His special nation Israel and He also loves and cares for all people who come to Him through Jesus Christ.

Thank God that you are loved and precious to Him. 

ALHAMISI TAREHE 19 APRILI 2018 ASUBUHI                                        

ISAYA 43:1-7

1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. 
Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 
Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. 
Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; 
nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. 
Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. 

Mungu anaongea na Waisraeli kupitia Nabii Isaya. Waisraeli wakati ile walikuwa utumwani kwa sababu ya dhambi na uasi wao. Mungu sasa anawaahidi kuwakusanya tena na kuwatunza.

Mungu anapenda taifa la Israeli na pia anapenda kila mtu anayekuja kwake kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo.

Mshukuru Mungu kwa upendo wake na utunzaji wake kwako.