Date: 
20-05-2017
Reading: 
GENESIS 16:1-5 (NIV)

Saturday 20th May 2017

WHEN YOU CRAVE FOR A NEW SONG: BLESSINGS WITH SORROW

GENESIS 16:1-5

Hagar and Ishmael

1 Now Sarai, Abram’s wife, had borne him no children.But she had an Egyptian slave named Hagar; so she said to Abram, “The Lord has kept me from having children. Go, sleep with my slave; perhaps I can build a family through her.”

Abram agreed to what Sarai said. So after Abram had been living in Canaan ten years, Sarai his wife took her Egyptian slave Hagar and gave her to her husband to be his wife. He slept with Hagar, and she conceived.

When she knew she was pregnant, she began to despise her mistress. Then Sarai said to Abram, “You are responsible for the wrong I am suffering. I put my slave in your arms, and now that she knows she is pregnant, she despises me. May the Lord judge between you and me.”

 

When searching for a new song a lot of people have gotten their fingers burnt in a place of seeking an alternative to God's promise. When God's promise is seemingly delayed, some Christians do not have the strength of character to keep waiting on the Lord and holding on to His promise; they therefore seek out and accept man's alternative to God's precious promises. These alternatives not only take you off God's course but also provide you with quick fixes that cannot really fix any anything, only a momentary joy that cannot absolve you of sorrow! It happened to Sarah when she could not conceive; she gave Hagar to Abraham, to bear children through her. But her relief turned into grief as her happiness became sorrow. At Genesis 16:4 the Bible says; 

" And he went into Hagar and she conceived and when she saw that she conceived, her mistress was despised in her eyes "

When you get tired of waiting for God's will, plan or promise to materialise, and you decide to follow one of the alternatives that come your way, you will only be hurting yourself. May you not use your own hands to undo yourself. When God blesses you, He removes every form of sorrow from it ( Proverb 10:22), but whatever blessing you believe can derive from substituting God's plan with an alternative will only be shot-lived and will definitely come to sorrow. Take time to find what is God's will for you in every area of your life and patiently follow it. You will have peace and prosperity coming after you!

UNAPOUTAFUTA WIMBO MPYA:TAHADHARI NA MAJUTO

MWANZO 16:1-5

1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. 
2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. 
3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. 
4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. 
5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.

 

Watu wengi huumia sana  wakitafuta na kufuata mbadala wa mpango ambao  Mungu ameupanga juu yake. Ahadi za Mungu kwetu  ni kweli na adili ila Wakristo wengi hukosa uvumilivu wa kusubiri kudhihirika kwa mpango wa Mungu na kuishia kutafuta mpango mbadala ambao matokeo yake ni hasara na majuto mengi. Sarah aliahidiwa kuwa mama wa taifa kubwa, akiwa bado hana mtoto. Akaangalia hali yake ya uzee na muda unavyokwenda akaona heri achomeke mpango wake, akamkabidhi mumewe Ibrahim, mjakazi wake Hajiri. Na Hajiri alipata mtoto, lakini furaha ya Sarah ilikuwa fupi sana, na kugeuka msiba, baada ya kitambo kidogo. Neno linatuambia katika Mwanzo 16:4,

    " Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake".

Ni pale ambapo unachoka kusubiri kudhihirika kwa mpango wa Mungu juu yako, ukaanza kuwa na mikakati yako, na kutafuta mbadala, ndiyo chanzo cha kuumia kwako kunapoanza, lazima utajiumiza mwenyewe. Mungu anapoamua baraka juu yako  haleti baraka na majuto (Mithali 10:22), kwake ni faraja tupu. Na pale unapoona unapata faraja toka katika hiyo mipango yako mwenyewe, mara zote ni faraja ya kitambo kidogo sana. Lazima majuto yataandamana nayo. Jitahidi sana usijiumize mwenyewe. Jitahidi sana kuutafuta mpango wa Mungu juu yako, na kuufuata kwa saburi  na bidii. Hakika amani na mafanikio vitakufuata.