Date: 
05-01-2018
Reading: 
Deuteronomy 6:20-25 (KUMBUKUMBU LA TORATI   6:20-25)

FRIDAY 5TH JANUARY 2018 MORNING                                  

Deuteronomy 6:20-25 New International Version (NIV)

20 In the future, when your son asks you, “What is the meaning of the stipulations, decrees and laws the Lord our God has commanded you?”21 tell him: “We were slaves of Pharaoh in Egypt, but the Lord brought us out of Egypt with a mighty hand. 22 Before our eyes the Lord sent signs and wonders—great and terrible—on Egypt and Pharaoh and his whole household. 23 But he brought us out from there to bring us in and give us the land he promised on oath to our ancestors. 24 The Lord commanded us to obey all these decrees and to fear the Lord our God, so that we might always prosper and be kept alive, as is the case today. 25 And if we are careful to obey all this law before the Lord our God, as he has commanded us, that will be our righteousness.”

As we read the instructions which God gave to the Israelites we too can learn something. It is good to remember history and to see how God has worked in the lives of our ancestors and how He has worked in our own lives. We should keep a record of these important events. Also it is important to teach our children about our faith.  Let each of us be faithful in living for God and in teaching our beliefs to the next generation.  

IJUMAA TAREHE 5 JANUARI 2018 ASUBUHI   

KUMBUKUMBU LA TORATI   6:20-25

20 Na zama zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N'nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza Bwana, Mungu wetu? 
21 Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; Bwana, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; 
22 Bwana akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; 
23 akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu. 
24 Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo. 
25 Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya Bwana, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

Tukisoma maagizo ya Mungu kwa Waisraeli sisi Wakristo wa leo pia tunayo ya kujifunza. Kwanza ni umuhimu wa kutunza historia ya kanisa na familia, na hasa kukumbuka matendo makuu ya Mungu katika maisha yetu. Pia tunapaswa kuwa na bidii kuwafundisha wototo wetu na vizazi vijavyo kwa ujumla.

Tusishindwe kuishi Kikristo na kurithisha imani yetu kwa watoto na vijana.