Date: 
02-01-2023
Reading: 
Ayubu 8:8-22

Jumatatu asubuhi tarehe 02.01.2022

Ayubu 8:8-22

[8]Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, 

Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

[9](Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, 

Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

[10]Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, 

Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

[11]Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope 

Na makangaga kumea pasipo maji?

[12]Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, 

Hunyauka mbele ya majani mengine.

[13]Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; 

Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

[14]Uthabiti wake utavunjika, 

Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.

[15]Ataitegemea nyumba yake, isisimame; 

Atashikamana nayo, isidumu.

[16]Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, 

Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.

[17]Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, 

Huangalia mahali penye mawe.

[18]Lakini, aking’olewa mahali pake, 

Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.

[19]Tazama, furaha ya njia yake ni hii, 

Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.

[20]Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, 

Wala hatawathibitisha watendao uovu.

[21]Bado atakijaza kinywa chako kicheko, 

Na midomo yako ataijaza shangwe.

[22]Hao wakuchukiao watavikwa aibu; 

Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.

Anza yote katika jina la Yesu Kristo;

Baada ya Ayubu kupitia mateso mengi akapoteza familia na mali, sura ya saba inamuonesha Ayubu akisema mateso yake hayana mwisho. Sura ya nane (somo la asubuhi hii) ananukuliwa Bildad akimwambia Ayubu kwamba anahitaji kutubu kwa sababu alinena isivyostahili. Akimpinga Ayubu, mstari wa 20 unaeleza Bwana alivyo kwa watu wake;

Ayubu 8:20

[20]Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, 
Wala hatawathibitisha watendao uovu.

Tayari tuko katika mwaka mpya wa 2023 kwa neema ya Mungu. Kuna uwezekano katika mwaka uliopita tulipitia shida na tabu, ambazo zinaweza kusababisha tuone kama vile mateso yetu hayana mwisho. Lakini kumbe tufahamu ya kuwa Mungu hatutupi, yuko nasi. Tuendelee kumtumaini katika yote, sasa na hata milele.

Furahia mwaka mpya kwa jina la Yesu.