Wazee wa Baraza Watembelea Mtaa wa Tabora

Wazee wa Baraza wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral tarehe 9 Julai 2022 walifanya ziara katika mtaa wa Tabora ili kujionea maendeleo ya mtaa huo na mradi wa ujenzi wa nyumba ya ibada unavyoendelea mtaani hapo. Wakiwa katika mtaa huo Wazee wa Baraza walipata maelezo mafupi juu ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya ibada

kutoka kwa mhandisi wa mradi huo. Katika maelezo yake mhandisi huyo alisema mradi utakamilika mnamo mwezi Oktoba mwaka huu iwapo hakutakuwa na changamoto za upatikanaji wa vifaa na fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemuiliyobakia.

Azania Front Cathedral Yaadhimisha miaka 12 ya Uhusiano na jiji la Hamburg

Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral mnamo tarehe 1 Julai 2022 uliandaa tamasha la uimbaji lililofanyika usharikani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 12 ya ushirikiano kati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania na jiji la Hamburg, Ujerumani.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wageni waliowakilisha jiji la Hamburg ambapo kwaya zote za usharika wa Kanisa Kuu zilipata kutumbuiza. Katika Tamasha hilo pia alihudhuria Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Mchungaji Charles Mzinga.

Washarika Azania Front Cathedral waaswa Kuzingatia Ushauri wa Madaktari

Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral hivi karibuni (Juni 25, 2022) iliandaa kambi ya matibabu (Afya Check) kwa ajili ya kupima na kutoa huduma za kitabibu kwa washarika na wananchi wote.

Kambi hiyo ya siku moja ilifanyika katika viwanja vya Usharika wa Azania Front ambapo zaidi ya wananchi 400 walihudhuria kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Azania Front Cathedral Yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2022

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, limeandaa utaratibu wa wanawake kuongoza ibada mara moja kwa mwaka, ibada hizi kwa kawaida hufanyika katika majira ya Kwaresma au mwezi Machi ambapo dunia huwa inaadhimisha siku ya wanawake duniani.

Kwa mwaka huu wa 2022, katika Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ibada ilifanyika tarehe 21/3/2022 ambapo wanawake waliongoza ibada zote zilizofanyika usharikani hapo siku hiyo.

Wanawake wa Usharika wa Azania Front Wahudhuria Semina

Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral hivi karibuni walihudhuria semina ya kiroho na kiuchumi. Semina hiyo ya siku moja ilifanyika tarehe 30/4/2022 katika kituo cha Consolata Mission Centre, Bunju Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya washarika wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral.

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuwaweka wanawake pamoja kwa ajili ya kupata mafundisho ya kiroho na kiuchumi, iliandaliwa na viongozi wa Umoja wa wanawake usharikani wakishirikiana na uongozi wa Usharika.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Azania Front Wafanyika

Wanawake wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral mnamo tarehe 19/3/2022 walikutana usharikani kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Umoja huo kwa mwaka 2022. Katika mkutano huo wanawake waliweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo na kanisa kwa ujumla.

Mkutano huo mkuu wa mwaka ulifunguliwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Mch Charles Mzinga ambaye katika salaam zake aliwataka washiriki kujadili kwa urefu na kutafuta suluhu juu ya chagamoto mbalimbali zinazoukabili umoja huo ili uweze kuimarika zaidi kwa maslahi mapana ya wanawake wa usharika na kanisa kwa ujumla.

Siku ya Vijana Usharika wa Azania Front Cathedral 2022

Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2022 ilikuwa ni Siku ya Vijana katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka ili kutambua na kuthamini mchango wa vijana katika kulijenga na kuliendeleza neno la Bwana.

Katika siku hiyo muhimu kwa vijana na usharika kwa ujumla, vijana wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front walipata fursa ya kuongoza ibada zote tatu za siku hiyo zilizoambatana na igizo kutoka kwa vijana hao.

Kwaya ya Agape Yawafariji Watoto Muhimbili Hospitali

Wanakwaya wa Kwaya ya Agape ya Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ambayo huimba katika ibada ya kwanza (saa moja asubuhi) siku za Jumapili, hivi karibuni walitembelea kitengo cha watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ziara hiyo ilifanyika tarehe 4/2/2022 ambapo kwaya hiyo iliweza kutoa kadi za bima ya afya kwa watoto wahitaji wapatao 64 na pia walitoa mahitaji mbalimbali kama nguo, sabuni, mafuta ya kupaka, miswaki, dawa za meno na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaopatiwa huduma za kitabibu hospitalini hapo.

Matangazo ya Usharika tarehe 7 Agosti 2022

MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 07 AGOSTI, 202

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MLANGO WA KUINGIA MBINGUNI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.

3. Matoleo ya Tarehe 31/07/2022     

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yak

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO

0757 391174 - KKKT AZANIA FRON

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRA