Date: 
01-07-2020
Reading: 
Acts 11:11-15

WEDNESDAY 1ST JULY 2020  MORNING                                            

Acts 11:11-15 New International Version (NIV)

11 “Right then three men who had been sent to me from Caesarea stopped at the house where I was staying. 12 The Spirit told me to have no hesitation about going with them. These six brothers also went with me, and we entered the man’s house. 13 He told us how he had seen an angel appear in his house and say, ‘Send to Joppa for Simon who is called Peter. 14 He will bring you a message through which you and all your household will be saved.’

15 “As I began to speak, the Holy Spirit came on them as he had come on us at the beginning. 

Peter emphasizes that what both the Gentiles and the Jewish believers hold in common is a gift from the Holy Spirit. His witness makes public his personal experience and his experience of others’ faith.

Sharing our experience with God and how He had transformed our lives can influence and change other people’s lives and result in the glorification of God.


JUMATANO TAREHE 01 JULAI 2020  ASUBUHI                   

MATENDO YA MITUME 11:11-15

11 Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.
12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
13 akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,
14 atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.
15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.

 

Mtume Petro anasisitiza kuwa jambo linalowaleta pamoja Wakristo wa Kiyahudi na wale wa Mataifa ni karama za Roho Mtakatifu. Ushuhuda wake unaeleza wazi jinsi Mungu alivyogusa imani yake na watu wengine.

Ikiwa tutawashuhudia wengine jinsi tulivyokutana na Mungu na akayabadili maisha yetu, maisha ya watu yataguswa na kubadilika na matokeo yake Mungu wetu atatukuzwa.