TUESDAY 28TH NOVEMBER 2017 MORNING
1 Thessalonians 1:3-10 New International Version (NIV)
3 We remember before our God and Father your work produced by faith, your labor prompted by love, and your endurance inspired by hope in our Lord Jesus Christ.
4 For we know, brothers and sisters[a] loved by God, that he has chosen you, 5 because our gospel came to you not simply with words but also with power, with the Holy Spirit and deep conviction. You know how we lived among you for your sake. 6 You became imitators of us and of the Lord, for you welcomed the message in the midst of severe suffering with the joy given by the Holy Spirit. 7 And so you became a model to all the believers in Macedonia and Achaia. 8 The Lord’s message rang out from you not only in Macedonia and Achaia—your faith in God has become known everywhere. Therefore we do not need to say anything about it, 9 for they themselves report what kind of reception you gave us. They tell how you turned to God from idols to serve the living and true God, 10 and to wait for his Son from heaven, whom he raised from the dead—Jesus, who rescues us from the coming wrath.
Footnotes:
- 1 Thessalonians 1:4 The Greek word for brothers and sisters (adelphoi) refers here to believers, both men and women, as part of God’s family; also in 2:1, 9, 14, 17; 3:7; 4:1, 10, 13; 5:1, 4, 12, 14, 25, 27.
The Apostle Paul thanks God for the Christians at Thessalonica. He is happy about their faith and their sanctification. They were waiting for the Second Coming of Christ.
Think about how you pray for your friends and family. Can you thank God for their faith?
JUMANNE TAREHE 28 NOVEMBA 2017 ASUBUHI
1 Thesalonike 1:3-10
3 Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.
4 Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;
5 ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
6 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.
7 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.
8 Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.
9 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;
10 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.
Mtume Paulo katika sala zake alimshukuru Mungu kwa imani ya Wakristo kule Thesalonike. Aliona imani yao katika Yesu Kristo na jinsi wanatakaswa na Roho Mtakatifu. Alijua kwamba walikuwa wanasubiri ujio wa pili wa Yesu Kristo.
Ukitazama marafiki na ndugu zako unaweza kumshuru Mungu kwa imani yao?