Date: 
25-09-2018
Reading: 
1 Samuel 16:11-16

TUESDAY 25TH SEPTEMBER 2018 MORNING              

1 Samuel 16:11-16 New International Version (NIV)

11 So he asked Jesse, “Are these all the sons you have?”

“There is still the youngest,” Jesse answered. “He is tending the sheep.”

Samuel said, “Send for him; we will not sit down until he arrives.”

12 So he sent for him and had him brought in. He was glowing with health and had a fine appearance and handsome features.

Then the Lord said, “Rise and anoint him; this is the one.”

13 So Samuel took the horn of oil and anointed him in the presence of his brothers, and from that day on the Spirit of the Lord came powerfully upon David. Samuel then went to Ramah.

David in Saul’s Service

14 Now the Spirit of the Lord had departed from Saul, and an evil[a] spirit from the Lord tormented him.

15 Saul’s attendants said to him, “See, an evil spirit from God is tormenting you. 16 Let our lord command his servants here to search for someone who can play the lyre. He will play when the evil spirit from God comes on you, and you will feel better.”

Footnotes:

  1. 1 Samuel 16:14 Or and a harmful; similarly in verses 15, 16 and 23

Here we see God choosing David as the Second King of Israel . The Prophet Samuel wanted to chose David’s  brother  Eliab to be king (1 Samuel 16:6). Even David’s Father Jesse discounted his youngest son. But David was the choice of God. God looks at the heart and not the outward appearance.

Pray that God would give you wisdom to make wise choices in your life.

JUMANNE TAREHE 25 SEPTEMBA 2018 ASUBUHI               

1 SAMWELI 16:11-16

 

 

11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. 
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. 
13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama. 
14 Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. 
15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. 
16 Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. 

 

Hapa tunaona jinsi Mungu alimchagua Daudi awe mfalme wa pili wa taifa la Israeli. Nabii Samweli alimwona kaka wa Daudi, Eliabu; alitaka kumchagua, lakini Mungu haitazami muonekano wa nje wa mtu, bali moyo wake (1 Samweli 16:6-7). Hata baba yake Daudi hakumhesabu kama anafaa lakini alikuwa uchaguzi wa Mungu.

Mungu atuongoze katika maamuzi yote ili tuchague kwa busara.