Date: 
24-01-2017
Reading: 
1 Corinthians 3:16-23 New International Version (NIV)

TUESDAY 24TH JANUARY 2017 MORNING                         

1 Corinthians 3:16-23 New International Version (NIV)

16 Don’t you know that you yourselves are God’s temple and that God’s Spirit dwells in your midst? 17 If anyone destroys God’s temple, God will destroy that person; for God’s temple is sacred, and you together are that temple.

18 Do not deceive yourselves. If any of you think you are wise by the standards of this age, you should become “fools” so that you may become wise. 19 For the wisdom of this world is foolishness in God’s sight. As it is written: “He catches the wise in their craftiness”[a]20 and again, “The Lord knows that the thoughts of the wise are futile.”[b] 21 So then, no more boasting about human leaders! All things are yours,22 whether Paul or Apollos or Cephas[c] or the world or life or death or the present or the future—all are yours, 23 and you are of Christ, and Christ is of God.

Footnotes:

  1. 1 Corinthians 3:19 Job 5:13
  2. 1 Corinthians 3:20 Psalm 94:11
  3. 1 Corinthians 3:22 That is, Peter

We have the joy of being Christians. The Holy Spirit lives in us so that we are God’s temple. Let us thank God for this and live our lives to please Him. Let us not trust in human wisdom or think that we are better than others. Let us be thankful and give all the glory to God.

JUMANNE TAREHE 24 JANUARI 2017 ASUBUHI                   

1 KORINTHO 3:16-23

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. 
18 Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. 
19 Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. 
20 Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili. 
21 Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; 
22 kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 
23 nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

Sisi tunafuraha kuwa Wakristo. Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu. Sisi ni hekalu la Mungu. Yote hii ni neema ya Mungu. Tusijisifu au kuona kwamba sisi ni bora kuliko watu wengine. Bali tumshukuru Mungu na tumpe Mungu sifa zote.