Date: 
03-01-2022
Reading: 
Zaburi 90:1-12

Jumatatu asubuhi tarehe 03.01.2022

Zaburi 90:1-12

1 Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.

2 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

3 Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu.

4 Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.

5 Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo.

6 Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka.

7 Maana tumetoweshwa kwa hasira yako, Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.

8 Umeyaweka maovu yetu mbele zako, Siri zetu katika mwanga wa uso wako.

9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.

10 Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.

11 Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?

12 Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.

Waliomngojea Mwokozi wamuona;

Wimbo tuliousoma (zaburi) ni sala ya shukrani inayotambua ukuu wa Mungu kwa kumuumba, kumlinda na kumtunza mwanadamu. Mungu ndiye amekuwa makao ya watu wake siku zote. Huwasamehe wanapotubu, hana hasira.

Zaburi hii inatukumbusha kukaa kwa Bwana, maana yeye ndiye makao yetu, ambaye hututunza na kutusamehe dhambi zetu. Siku zetu zitakuwa za neema, na kuepuka ghadhabu ya Mungu. Tusichoke kukaa kwa Bwana, maana ndipo kwenye usalama wetu. Tuendelee kumngojea Bwana, tutamuona.