Date: 
15-10-2021
Reading: 
Yoshua 10:12-14

Ijumaa asubuhi 15.10.2021

Yoshua 10:12-14

[12]Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, 

Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; 

Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

[13]Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, 

Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. 

Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima.

[14]Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.

 

Nguvu ya Imani katika Yesu Kristo;

Yoshua aliomba jua na mwezi vikasimama, hadi pale Israeli walipokuwa wamejipatiliza juu ya adui zao. Tunaona kuwa katika siku za Yoshua, haikuwai kutokea hivyo, na hata baada ya siku hiyo, haikutokea.

Yoshua anadhihirisha imani yake kwa Mungu. Aliomba kwa Imani. Katika waraka wa Yakobo tunasisitizwa kuomba kwa imani;

Yakobo 5:15

[15]Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

Tunapoomba tuwe na imani kwa Yesu Kristo, yaani tumwombe tunayemwamini. Yeye hutusikia na kutupa mahitaji yetu, maana ndiye aliyetuita tumwamini.

Siku njema.