Date: 
08-01-2022
Reading: 
Yohana 9:1-5

Jumamosi asubuhi tarehe 08.01.2022

Yohana 9:1-5

1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.

2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?

3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.

4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.

5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.

Yesu ni nuru ya Ulimwengu;

Sura ya 9 ya Yohana inaeleza jinsi Yesu alivyomponya kipofu. Ilileta shida, mafarisayo wakamuuliza maswali ya kutosha yule aliyeponywa, hadi wazazi wake. Mwisho wake yule aliyeponywa akasema "..nilikuwa kipofu, sasa naona..". 

Yesu alikuwa anautangaza ufalme wake, kuwa alikuja kuwaokoa wenye dhambi. Kipofu ni alama ya wenye dhambi wanaohitaji wokovu. Sisi tu vipofu (tu wenye dhambi) tunaohitaji msamaha wa dhambi siku zote. Tuishi maisha ya toba. Kubaki dhambini ni kuwa kipofu. 

Jumamosi njema.