Date: 
12-02-2022
Reading: 
Yohana 11:38-44

Jumamosi asubuhi tarehe 12.02.2022

Yohana 11:38-44

38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.

39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.

40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?

41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Yesu alimfufua Lazaro aliyekuwa tayari kaburini, akiwa na siku nne amekufa. Martha alikuwa na wasiwasi wa ndugu yake kufufuka, lakini Yesu anamjibu;

Yohana 11:40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?

Ujumbe wa leo asubuhi ni kumwamini Yesu ili tuuone utukufu wa Mungu. Utukufu wa Mungu ni nafasi yake, na kazi zake. Basi tukimwamini na kumtegemea Yesu tutauona utukufu wake, yaani tutafanikiwa katika yeye na kuurithi uzima wa milele.

Siku njema.