Date: 
18-09-2021
Reading: 
Yeremia 11:18-23

Jumamosi tarehe 18 Septemba 2021, asubuhi 

Yeremia 11:18-23

[18]Tena BWANA akanijulisha haya, nami nikayajua; ndipo uliponionyesha matendo yao.

[19]Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.

[20]Lakini, Ee BWANA wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.

[21]Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la BWANA, usije ukafa kwa mkono wetu.

[22]Kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa;

[23]wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao.

 

Mungu hujishughulisha na mambo yetu;

Maisha ya Yeremia yako hatarini, lakini yeye anamuita Mungu aliye hai, Bwana wa majeshi kumnusuru. Tunasoma Mungu akiwa na Yeremia, akiahidi kuwaadhibu wanaotishia na Yeremia.

Ujumbe unaoletwa kwetu kwa somo hili ni kumuita Bwana pale tuonapo usalama wetu uko hatarini. Uhakika anaotoa Bwana ni kuleta mabaya juu ya wale watishiao usalama wetu. Hivyo tuko salama, kwa msaada wa Bwana.

Siku njema.