Date: 
15-01-2022
Reading: 
Warumi 14:8-9

Jumamosi asubuhi tarehe 15.01.2022

Warumi 14:8-9

8 Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.

9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.

Wabatizwao ndio wana wa Mungu;

Asubuhi ya leo tunasoma Mtume Paulo akitukumbusha juu ya maisha yetu, kuwa kuishi na kufa kwetu ni katika Bwana, ndiyo maana katika kuishi na kufa tu mali ya BWANA. Hii ni kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka kwa ya ajili ya walio hai na waliokufa.

Ubatizo unatufanya tuzaliwe katika Kristo, hivyo kuishi na kufa katika Kristo. Hivyo ni muhimu kuishi ahadi ya ubatizo wetu, ili tuwe mali ya BWANA, yaani tuishi katika Bwana, na kufa katika Bwana.

Jumamosi njema.