Event Date: 
14-03-2022

Kila mwaka wanawake wote wa kikristo duniani, huungana na kufanya maombi kwa pamoja kwa kuombea amani duniani, ushirikiano, upendo, kuombea familia na kazi za kanisa, maombi haya huandaliwa na nchi iliyoteuliwa kwa kupata zamu ya kuandaa.

Mwaka huu  maombi hayo yaliandaliwa na wanawake wa nchi ya Uingereza, katika mkoa wa Dar es Salaam, maombi hayo yalifanyika siku ya Ijumaa tarehe 4/3/2022 katika viwanja Saba Saba ambayo yalisimamiwa na dhahebu la Baptist, Wanawake wengi walishiriki maombi hayo wakitokea katika madhehebu mbalimbali ya kikristo likiwemo dhehebu la Kilutheri.

Wanawake wa Usharika wa Azania Front Cathedral wakishiriki katika ibada ya maombi ya dunia tarehe 4/3/2022

------------------------------------

Ripoti hii imeandaliwa na Jane Mhina