Date: 
17-01-2023
Reading: 
Wakolosai 3:8-25

Jumanne asubuhi tarehe 17.01.2023

Wakolosai 3:18-25

[18]Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.

[19]Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

[20]Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.

[21]Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

[22]Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.

[23]Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,

[24]mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

[25]Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;

Mtume Paulo anawaandikia Wakolosai akiwapa mawaidha ya familia. Anawaandikia watu katika nyumba, yaani familia iwapasavyo kutenda, kila mmoja kwa nafasi yake. Akina baba wanaagizwa kuwapenda wake zao, wake kuwatii waume zao, watoto kuwatii wazazi wao, watumwa kuwatii mabwana zao. 

Kila mmoja wetu anakumbushwa kutimiza wajibu wake katika familia. Kila mtu anaalikwa kuwajibika. Kutimiza wajibu ni kumcha Bwana ili kupata baraka katika familia zetu. Yote tufanyayo, tufanye katika Bwana tukitimiza wajibu katika nyumba zetu, hili ni agizo.

Siku njema