Date: 
09-11-2021
Reading: 
Waebrania 12:1-3

Jumanne asubuhi tarehe 09.11.2021

Waebrania 12:1-3

[1]Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
 
[2]tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
 
[3]Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

 

Uenyeji wa mbinguni;

Baada ya maelezo kuhusu imani (sura ya 11), sura ya 12 inamuelezea Yesu Kristo kama mwanzilishi wa imani yetu kwa jinsi alivyoustahimili msalaba bila aibu, ili katika yeye wote waokolewe.

Hivyo tunaitwa kumfuata Yesu, maana yeye ndiye sababu ya imani yetu, na ameketi kwenye kiti cha enzi akitungojea. Tudumu katika msingi uleule ambao kwao tuliamini, ili tumuone Yesu kwenye kiti cha enzi. 

Siku njema.