PICHA NA HABARI ZA MTAA WA VIWEGE UNAOTUNZWA NA AZANIAFRONT  

Washarika katika mtaa wa Viwege wakifuatilia Ibada iliyoendeshwa na Mchungaji Prudence Chuwa kutoka Usharika wa Kanisa Kuu, Azaniafront. Ibada hiyo ilifanyika tarehe 19/08/2018. Picha na Paulin Paul/AZF

Mchungaji Prudence Chuwa akiendesha Ibada ya Ubatizo katika mtaa wa Viwege. Jumla ya watoto nane pamoja na watu wazima wawili walibatizwa ikiwa ni pamoja na kurudisha kundini washarika sita. Picha na Paulin Paul/AZF

Mchungaji Prudence Chuwa (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika moja ya miradi ya ujenzi inayoendelea katika mtaa wa Viwege. Hapa ni mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Shule ya Jumapili (Sunday School). Kwa sasa nyumba ya Mwinjilisti Laban Mnzava (pichani: wa nne kutoka kushoto) ndiyo inayotumika kuwafundishia watoto katika mtaa huu. Picha na Paulin Paul/AZF