Event Date: 
21-11-2015

Vijana ambao walikuwa wanafunzi wa Sunday school, siku ya Jumamosi tarehe 21.11.2015 walibarikiwa rasmi kuanza kuhudhuria ibada ya watu wazima baada ya kufuzu mafunzo ya kipaimara waliyosoma kwa muda wa mika miwili, Msaidizi wa Askofu Chediel Lwiza ndie aliyeongoza ibada hiyo akishirikiana na na Mchungaji Kiongozi Charles Mzinga, na Mchungaji Prudence Chuwa.

Mch. Lwiza alisema "Kuanzia leo mtakuwa mnaongozana na wazazi wenu na kuingia nao katika ibada ya watu wazima. Sasa, mnachotakiwa kiukifanya ni kujifunza neno la mungu na kulijua, mkikwama muonane na mchungaji ama waalimu wenu wa zamani wa sunday school, pia mnatakiwa kujiunga na kwaya mbalimbali ambazo zinahudumu hapa kanisani kwa sababu nyinyi sio watoto tena bali ni vijana"

Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na wazazi na walezi, walimu wa sunday school na washarika mbalimbali.

Pia katika ibada hiyo kulikuwa na ubatizo wa mtoto mdogo mmoja na vijana wawili. Mambo yalikua kama ifuatavyo katika picha.

2015kipaimara 02

Msaidizi wa Askofu Mch. Chediel Lwiza, Mch. Prudence Chuwa, Mch. Kiongozi Charles Mzinga na watoto wakiingia ibadani kwa

maadamano

2015kipaimara 03

Vijana waliohitimu mafunzo ya kipaimara wakifuatilia ibada

2015kipaimara 05

Vijana walioitimu mafunzo ya kipaimara wakifutilia ibada

2015kipaimara 06

Baadhi ya Wazazi na Washarika wakifuatilia ibada ya kipaimara kwa makini

2015kipaimara 07

2015kipaimara 08

Mchungaji Charles Mzinga akiendesha ibada ya kipaimara

2015kipaimara 09

Msaidizi wa Askofu Mch. Lwiza akiwabariki vijana

2015kipaimara 10

2015kipaimara 11

2015kipaimara 12

Kijana akikabidhiwa moja ya Biblia zilizopewa vijana wote waliobarikiwa

2015kipaimara 13

2015kipaimara 15

Mch. Chuwa akitoa mahubiri

2015kipaimara 16

Wachungaji wote 3 wakiendelea na ibada

2015kipaimara 17

2015kipaimara 19

Mch. Lwiza akibariki Divai ya Sakramenti ya meza ya Bwana

2015kipaimara 20

Mch. Mzinga Akibariki mkate wa Sakramenti2015kipaimara 21

Parish worker Mama Urasa Akihudumu2015kipaimara 22

Vijana washiriki Meza ya Bwana kwa mara ya kwanza

2015kipaimara 23

Kijana na Msharika wakishiriki

2015kipaimara 25

Watumishi wakishiriki

2015kipaimara 26

Vijana wakionyesha vyeti vyao vya kipaimara

2015kipaimara 27

Kikundi cha Matumbeta wakihudumu

2015kipaimara 28

Mwalimu Abisai akihudumu

2015kipaimara 29

Mwalimu wa ibada ya kiswahili Jane Mhina akiwa sambamba na Parish Worker Urasa wakifuatilia ibada ya kipaimara.

2015kipaimara 30

1Vijana 2 ambao pia waliobatizwa siku hiyo, wakiwa na wasimamizi wao wakisubiri kubatizwa

2015kipaimara 31

Kijana akibatizwa

2015kipaimara 32

1Msaidizi wa askofu Mch Chediel Lwiza akiwabariki wazazi wa mtoto aliyebatizwa.

2015kipaimara 33

1Kijana akitoa zawadi ya shukrani kwa Usharika kwa niaba ya vijana wote waliobarikiwa siku hiyo.

2015kipaimara 34

 

2015kipaimara 35

Msaidizi wa Askofu na wachungaji wakifunga ibada.

2015kipaimara 36

Mch. Lwiza akitoa baraka.

2015kipaimara 38

Mchungaji Charles Mzinga akisema jambo kabla ya mwisho wa ibada.

2015kipaimara 39

 Kikundi cha matarumbeta wakiongoza ibada kutoka nje kwa maadamano

2015kipaimara 40

1Mchungaji Prudence Chuwa akimpongeza kijana aliyepata kipaimara

2015kipaimara 41

1Msaidizi wa askofu akiwa ameambatana na Mchungaji Prudence Chuwa akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliopata kipaimara

sambamba na wazazi wao.

2015kipaimara 42

1Mchungaji Charles Mzinga akimpa mkono wa amani Mchungaji Prundece Chuwa baada ya ibada kumalizika.

2015kipaimara 43

Vijana waliobarikiwa wakiwa katika picha ya pamoja.

2015kipaimara 44

Wana Matarumbeta wakiwa nje ya kanisa kufunga ibada.

2015kipaimara 46

 2015kipaimara 48

Mch. Mzinga akiteta jambo na mpiga tarumbeta.

(Picha na habari na Jane Mhina)