Date: 
08-11-2021
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 22:1-5 (Revelations)

JUMATATU TAREHE 8 NOVEMBA 2021, ASUBUHI.

Ufunuo wa Yohana 22:1-5

1 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;

4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

Uenyeji wa mbinguni;

Yohana kabla ya kuhitimisha ufunuo wake, anaoneshwa mto wa maji ya uzima kutoka kiti cha enzi cha Mungu na Mwana-Kondoo. Anaoneshwa sehemu yenye raha kwa watakatifu wakakaouingia ufalme wa Mungu. Yohana anaoneshwa mbingu ambayo watakaoingia watamwona Bwana, akitawala milele.

Wajibu wetu ni kutafakari, kwamba tumejiandaa vipi kuuingia mji huu ambao Yohana anaoneshwa. Tafakari kama mwenendo wako utakuingiza mbinguni.

Uwe na wiki njema


MONDAY, NOVEMBER 8, 2021, MORNING.

Revelation 22: 1-5 (NIV)

Eden Restored

1 Then the angel showed me the river of the water of life, as clear as crystal, flowing from the throne of God and of the Lamb down the middle of the great street of the city. On each side of the river stood the tree of life, bearing twelve crops of fruit, yielding its fruit every month. And the leaves of the tree are for the healing of the nations. No longer will there be any curse. The throne of God and of the Lamb will be in the city, and his servants will serve him. They will see his face, and his name will be on their foreheads. There will be no more night. They will not need the light of a lamp or the light of the sun, for the Lord God will give them light. And they will reign for ever and ever.

Read full chapter

Citizenship of Heaven;

Before concluding his revelation, John is shown a river of water of life from the throne of God and of the Lamb. He is shown a comfortable place for the saints who have entered the kingdom of God. John is shown a heaven in which those who enter will see the Lord, ruling forever.

Our responsibility is to reflect, on how we are prepared to enter this city in which John is shown. Contemplate this notion as you interact with others in your life.

Have a great week