Date: 
29-06-2022
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 21:1-4

Jumatano asubuhi 29.06.2022

Ufunuo wa Yohana 21:1-4

1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Wito wa kuingia ufalme wa Mungu;

Yohana anafunuliwa juu ya mbingu na nchi mpya, na siyo ile ya zamani. Ni Yerusalemu mpya mji ulioandaliwa kwa ajili ya wateule. Katika hii mbingu mpya, Mungu anaahidi kufanya maskani na watu wake waliomwamini, ambao atawafuta machozi baada ya kushinda hapa duniani.

Yohana anafunuliwa juu ya maisha yajayo baada ya hapa duniani. Tumejiandaaje kwa maisha yajayo? Tujiandae kwa kutenda yatupasayo katika imani, ndipo Yesu atatufuta machozi hivyo kuingia katika ufalme wake.

Siku njema.