Kwaya ya akinamama Kanisa Kuu la Azania Front imekuwa ikishiriki katika uimbaji kwa

miaka mingi.Uimbaji huu umekuwa ukifanyika katika ibada, matamasha mbalimbali, mialiko,

kufarijiana pamoja na kutembelea wagonjwa mahospitalini. Uongozi wa kwaya hii huchaguliwa

kila baada ya miaka minne. Uongozi uliopita ulianza mwezi wa Julai 2010 na kumaliza muda wake

mwezi wa Juni 2014. Viongozi wapya kwa kipindi cha kuanzia Julai 2014 mpaka Juni 2018 walichaguliwa

tarehe 02-07-2014 nao ni kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti - Eileen Mavura

Makamu - Anna Kaduri

Katibu - Freda Bgoya

Katibu Msaidizi - Mary Matoi

Mtunza Hazina - Omega Mongi

Mtunza Hazina - Angela Malyi.

uchaguzi01

Wajumbe wakimsikiliza mratibu wa uchaguzi

¦

uchaguzi02

Waratibu wa uchaguzi, Stella Sykes wa kamati ya malezi (kushoto) na Theodus msangi wa kamati ya Uinjilisti

¦

uchaguzi03

Wajumbe wakipiga kura

¦

uchaguzi06

¦

uchaguzi12

Waratibu wakitangaza matokeo

¦

uchaguzi11

Viongozi wapya wakiwa na nyuso za furaha na waratibu wa uchaguzi.