Date: 
11-01-2017
Reading: 
Romans 6:3-11 (NIV)

WEDNESDAY 11TH JANUARY 2017 MORNING              

Romans 6:3-11 New International Version (NIV)

Or don’t you know that all of us who were baptized into Christ Jesus were baptized into his death? We were therefore buried with him through baptism into death in order that, just as Christ was raised from the dead through the glory of the Father, we too may live a new life.

For if we have been united with him in a death like his, we will certainly also be united with him in a resurrection like his. For we know that our old self was crucified with him so that the body ruled by sin might be done away with,[a] that we should no longer be slaves to sin— because anyone who has died has been set free from sin.

Now if we died with Christ, we believe that we will also live with him.For we know that since Christ was raised from the dead, he cannot die again; death no longer has mastery over him. 10 The death he died, he died to sin once for all; but the life he lives, he lives to God.

11 In the same way, count yourselves dead to sin but alive to God in Christ Jesus.

Footnotes:

  1. Romans 6:6 Or be rendered powerless

Baptism is the foundation of our lives as Christians. It is like a new beginning. In baptism we bury the old life of sin and rise again to be a new spiritual person.  We should continue this process by turning away from sin. We need to refuse sinful desires and allow Christ to rule in our lives. 

JUMATANO TAREHE 11 JANUARI 2017 ASUBUHI               

RUMI 6:3-11

3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 
5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 
6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 
7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. 
8 Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; 
9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. 
10 Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. 
11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. 
 

Ubatizo ni msingi wa maisha yetu kama wakristo. Katika Ubatizo tunaanza maisha upya kiroho. Tunapaswa kuzika mwili wa asili wenye dhambi na kufufuka na Yesu Kristo. Tunapaswa kujitahidi kila siku kukataa dhambi na kuishi maisha  yakiongozwa na Yesu Kristo.