Date: 
15-01-2020
Reading: 
Romans 6:1-11

WEDNESDAY 15TH JANUARY 2020 MORNING                                                

Romans 6:1-11 New International Version (NIV)

Dead to Sin, Alive in Christ

1 What shall we say, then? Shall we go on sinning so that grace may increase? By no means! We are those who have died to sin; how can we live in it any longer? Or don’t you know that all of us who were baptized into Christ Jesus were baptized into his death? We were therefore buried with him through baptism into death in order that, just as Christ was raised from the dead through the glory of the Father, we too may live a new life.

For if we have been united with him in a death like his, we will certainly also be united with him in a resurrection like his. For we know that our old self was crucified with him so that the body ruled by sin might be done away with,[a] that we should no longer be slaves to sin— because anyone who has died has been set free from sin.

Now if we died with Christ, we believe that we will also live with him. For we know that since Christ was raised from the dead, he cannot die again; death no longer has mastery over him. 10 The death he died, he died to sin once for all; but the life he lives, he lives to God.

11 In the same way, count yourselves dead to sin but alive to God in Christ Jesus. 

By God’s grace we have been united with Christ, that our old nature was broken when Christ died. We now share the power of Christ's life in our lives. We must believe this enough to live our lives according to God’s will.


JUMATANO TAREHE 15 JANUARI 2020 ASUBUHI                               

WARUMI 6:1-11

1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;
tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.
10 Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.
11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Kwa neema ya Mungu tumeunganishwa na Kristo, na kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja naye. Sasa tunayo nguvu ya uzima wa Kristo maishani mwetu. Tunapaswa kuamini hivyo ili tuishi kama Mungu alivyokusudia.