MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 25 MEI, 2025

SIKU YA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA (CCT)

NENO LINALOTUONGOZA NI  

NDUGU WAKAE PAMOJA KWA UMOJA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliyeotufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 18 /05/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 18/05/2025 ni Washarika 613. Sunday School 226

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

4. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika Karibuni.

8. Alhamisi ijayo tarehe 29/05/2025 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya kukumbuka kupaa kwa Yesu Kristo. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.

9. Tarehe 07/06/2025 saa 3.00 asubuhi Katika Usharika wa KKKT Mbezi Beach, kutakuwa na ibada maalum ya maombi kwa ajili ya waliohitimu kidato cha sita na wahitimu wengine. Ibada hii maalum inatambulika kama Mtoko wa Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa. Neno kuu: KAMA SI BWANA ALIYEKUWA PAMOJA NASI, ISRAELI NA ASEME SASA. Vijana walio hitimu pamoja na wazazi wao wanaombwa kushiriki kikamilifu. Washiriki wote wajiandikishe ofisi ya Mchungaji. Mwisho wa usajili ni tarehe 02/06/2025. Pia wazazi mnahimizwa kuwasajili pia watoto walioko shule za Bweni. 

10. Uongozi wa Shule ya Jumapili unapenda kuwatangazia Wazazi/Walezi kuwa Tamasha la uimbaji la watoto litafanyika mwezi wa sita. Sare watakayovaa itakuwa ni tshirt ambazo zimeandaliwa na Uongozi wa DMP. Tshirt moja ni sh. 12,000/=. Hivyo Wazazi na Walezi mnaombwa muwanunulie watoto ili waweze kuvaa siku hiyo ya tamasha. Mungu awabariki.

11. Uongozi wa Vijana kwa kushirikiana na jukwaa la wanaume wanawaletea Filamu ya “THE FORGE” by Kendrick Brothers Itakayofanyika Jumamosi ijayo tarehe 31 Mei 2025 Saa 12 Jioni Azania Front Cathedral (ndani ya kanisa). Mafunzo tarajiwa kupitia sinema hii ni Ufuasi wa Yesu Kristo, Wokovu, Msamaha, Kijana na Uwajibikaji, Nguvu ya maombi, Kwa maudhui ya sinema hiii yenye kulenga kuboresha nafasi ya vijana hasa Kijana wa Kiume katika jamii. Watu wa rika/umri na jinsia zote mnakaribishwa.

12. Kwaya ya Upendo leo wapo Dodoma kwa ajili ya huduma. Washarika tuwaombee washiriki ibada vizuri huko na warudi salama.

13. SHUKRANI -JUMAPILI IJAYO TAREHE 01/06/2025

KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Jacqueline Mapesa pamoja na wadogo zake Mary na Moureen watamshukuru Mungu kwa Uzima, neema, kibali kati yao na katika kazi zao, uzima wa mama yao baada ya kuumwa kipindi kirefu, mdogo wao Moureen kufanya vizuri katika masomo yake pamoja na kuwatia nguvu tangu baba yao mpendwa Mapesa na ndugu zao walipotwaliwa na Bwana.

Neno: Zaburi 100:4, TMW 399,389

14. NDOA. Hakuna Ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.

15. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Lyimo
  • Upanga: Kwa Mama Maro
  • Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Prof. na Bibi Mashala
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Matandiko
  • Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Watatangaziana

16. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram

17. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza 

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.