Date: 
31-01-2018
Reading: 
Romans 3:27-31 NIV (Warumi 3:27-31}

WEDNESDAY 31ST JANUARY 2018 MORNING                     

Romans 3:27-31 New International Version (NIV)

27 Where, then, is boasting? It is excluded. Because of what law? The law that requires works? No, because of the law that requires faith. 28 For we maintain that a person is justified by faith apart from the works of the law. 29 Or is God the God of Jews only? Is he not the God of Gentiles too? Yes, of Gentiles too, 30 since there is only one God, who will justify the circumcised by faith and the uncircumcised through that same faith.31 Do we, then, nullify the law by this faith? Not at all! Rather, we uphold the law.

We are saved by Grace not by works. Jesus died for us to pay the punishment for our sins. We receive the gift of salvation by repentance and faith in Christ. We cannot earn our salvation by doing good works or obeying the law. However the law is good and shows us how God wants us to live.

JUMATANO TAREHE 31 JANUARI 2018 ASUBUHI               

WARUMI 3:27-31

27 Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. 
28 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. 
29 Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; 
30 kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. 
31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.

Tunaokolewa kwa Neema siyo kwa matendo. Yesu Kristo alitufia msalabani ili kulipa ahabu kwa ajili ya dhambi zetu. Tunapokea  zawadi ya wokovu kwa njia ya toba na kumwamini Yesu Kristo. Hatuwezi kupata wokovu kwa njia ya kutenda matendo mema au kutii sheria. Lakini sheria ni njema, na inatuonyesha jinsi Mungu anavyotaka tuishi.