Date: 
07-09-2020
Reading: 
Romans 13:8-10 (Warumi)

MONDAY 6TH SEPTEMBER 2020   MORNING                                              

Romans 13:8-10 New International Version (NIV)

Let no debt remain outstanding, except the continuing debt to love one another, for whoever loves others has fulfilled the law. The commandments, “You shall not commit adultery,” “You shall not murder,” “You shall not steal,” “You shall not covet,”[a] and whatever other command there may be, are summed up in this one command: “Love your neighbor as yourself.”[b] 10 Love does no harm to a neighbor. Therefore love is the fulfillment of the law.

The giving of love fulfills three purposes. First, it blesses the person who receives love because many people are desperately in need of a kind word or some small demonstration that someone cares about them. Second, the Christian who shows love for his/her neighbor becomes a powerful witness for Christ. Third, as Paul states next, love fulfills the law.


JUMATATU TAREHE 7 SEPTEMBA 2020  ASUBUHI                                

WARUMI 13:8-10

Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Tukionyesha upendo kwa wengine tunatimiza mambo matatu: Kwanza, humbariki yule anayepokea upendo kwa sababu watu wengi wanatafuta sana neno la ukarimu au kuona kuwa yupo mtu anayewajali, japo kidogo. Pili, Mkristo anayeonesha upendo kwa jirani yake anakuwa shahidi thabiti wa Kristo. Tatu, kama Mtume Paulo anavyoendelea kueleza kuwa, upendo huitimiza sheria yote.