Date: 
16-07-2017
Reading: 
Psalm : 73:24-28, John 1:11-13, Jeremiah 1:17-19 (NIV) Zaburi 73:24-28, Yohana 1:11-13, Yeremia 1:17-19

SUNDAY 16TH JULY 2017 5TH SUNDAY AFTER HOLY TRINITY

THEME : DISCIPLESHIP

Psalm : 73:24-28, John 1:11-13, Jeremiah 1:17-19

Psalm 73:24-28New International Version (NIV)

24 You guide me with your counsel,
    and afterward you will take me into glory.
25 Whom have I in heaven but you?
    And earth has nothing I desire besides you.
26 My flesh and my heart may fail,
    but God is the strength of my heart
    and my portion forever.

27 Those who are far from you will perish;
    you destroy all who are unfaithful to you.
28 But as for me, it is good to be near God.
    I have made the Sovereign Lord my refuge;
    I will tell of all your deeds.

 

John 1:11-13 New International Version (NIV)

11 He came to that which was his own, but his own did not receive him.12 Yet to all who did receive him, to those who believed in his name, he gave the right to become children of God— 13 children born not of natural descent, nor of human decision or a husband’s will, but born of God.

 

Jeremiah 1:17-19    New International Version (NIV)

17 “Get yourself ready! Stand up and say to them whatever I command you. Do not be terrified by them, or I will terrify you before them.18 Today I have made you a fortified city, an iron pillar and a bronze wall to stand against the whole land—against the kings of Judah, its officials, its priests and the people of the land. 19 They will fight against you but will not overcome you, for I am with you and will rescue you,” declares the Lord.

God called Jeremiah to be a prophet to take God’s messages to the people. Jeremiah was afraid and felt inadequate for the task . God promised to be with him and strengthen him for the task. God did not promise that it would be easy but He promised to be with Jeremiah.

What is God calling you to do? Are you willing to obey Him?

The place of blessing is to be in the centre of God’s will. Trust in Jesus and obey and follow Him always.  

JUMAPILI TAREHE 16 JULAI 2017 SIKU YA BWANA YA 5 BAADA YA UTATU

WAZO KUU: UFUASI NA UANAFUNZI

Zaburi 73:24-28, Yohana 1:11-13, Yeremia 1:17-19

Zaburi 73:24-28

24 Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu. 
25 Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. 
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele. 
27 Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe. 
28 Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.

 

Yohana 1:11-13

11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 
 

Yeremia 1:17-19

17 Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao. 
18 Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. 
19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.

Mungu alimwita Yeremia kuwa Nabii. Mungu alimwita kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu wake. Yeremia aliogopa na alijisikia udhaifu. Mungu aliahidi kuwa naye na kumsaidia. Mungu hakuahidi mambo yatakuwa rahisi lakini aliahidi kuwa pamoja na Yeremia.

Wewe je! Mungu amekuita kufanya nini? Upo tayari kumtii? Mahali pa baraka katika maisha yako ni kuwa katika mipango ya Mungu. Tafuta mapenzi ya Mungu kwa maisha yako na uyafuate.