DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 01 FEBRUARI, 2026

SIKU YA BWANA YA MWISHO KATIKA MAJIRA YA UFUNUO

NENO LINALOTUONGOZA NI

NEEMA YA MUNGU YATOSHA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 25/01/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 18/01/2026 ni Washarika 970 na Sunday School 285

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 01/02/2026 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

8. Kwaya ya Agape inawashukuru uongozi wa kanisa, Walezi kamati ya malezi na washarika wote waliowashika mkono katika Huduma wanayofanya kila mwaka pale MOI kwa watoto wenye mtindio wa ubongo kwa kuwalipia bima na mahitaji mbalimbali. Wanarudi tena kwenu washarika mwaka huu tukiendelea na huduma hii pale Muhimbili na tunatarajia kufika pia Ocean road hospital kuwasaidia watoto na wakubwa wanaohitaji matibabu kwa kadri Mungu wetu na washarika mtakavyotuwezesha. Tunaomba mtakaoweza kuleta mahitaji kama mafuta ya kujipaka,dawa za meno,sabuni ya kufulia au kuogea ,maji ya kunywa pampas,nguo nzuri za watoto na wakubwa lakini pia kulipia watoto Bima ya Afya ambayo kwa mtoto mmoja ni Tsh 150,000. Unaweza kuchangia kupitia kwenye Acc ya Maendeleo Bank No 013874006021 jina Agape Evangelical Singer Azania Front Au kwa njia ya simu Yaani M-Pesa namba 0767214441 jina Janice Kaisi. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwaona viongozi wa kwaya ya Agape. Mungu akubariki sana.

9. Idara ya sanaa na michezo inapenda kuwatangazia vijana wote kuwa mazoezi ya maandalizi ya igizo la pasaka yameanza, siku za mazoezi ni jumatatu saa 11:00 jioni na Jumamosi saa 10:00 jioni, Vijana wote mnakaribishwa kushiriki maandalizi ya Igizo hili . Aidha Kutakuwa na mtihani wa ufahamu wa Biblia, vijana wote mnakaribishwa kwenye maandalizi, siku za mazoezi ni Jumanne saa 11 jioni na alhamisi saa 11jioni. Mungu awabariki sana.

10. SHUKRANI: JUMAPILI TAREHE 08/02/2026

 IBADA ZOTE TATU

- Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote wa ibada zote 3 wajiandae kwa ajili ya sadaka ya kumshukuru Mungu aliyetulinda mwaka mzima,pamoja na mambo mengine mengi. Sadaka hiyo itatolewa jumapili ya tar 8/2/2027 vijana wote wajiandae

 Neno zab 9:1-2

 IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

- Mzee Mathias Kavuga na Mama Anna Kavugha, watamshukuru Mungu kwa kuhudumiwa na Usharika wa Azania Front Cathedral tokea February 1960 pamoja na mambo mengi aliyowatendea.

 Neno: Zaburi 121, Wimbo: KWAYA KUU (Kanisa langu la Kristo)

11. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

 KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 14/02/2026. NDOA HII ITAFUNGWA KKKT MOSHI MJINI KATI YA

  •  Bw. Cliffson Lord Macha na Bi Karen Edmund Maeda

 Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Upanga: Kwa Mzee Mbwilo. Mtaa wa Ismail

  • Mjini kati: Hapa usharikani saa moja kamili asubuhi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Adv. Jospeh na Adv. Vupe Mpuya

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

14. Zamu za wazee ni kundi la Kwanza .

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.