Date: 
31-01-2026
Reading: 
Amosi 3:4-7

Jumamosi asubuhi tarehe 31.01.2026 

Amosi 3:4-7

4 Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwana-simba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu?

5 Je! Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka juu ya nchi, bila kunasa kitu cho chote?

6 Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta Bwana?

7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Yesu ajidhihirisha katika utukufu wake;

Ujumbe tuliousoma ulikuwa kwa Israeli kwa sababu ya dhambi. Watu walikosa haki zao, huku rushwa, uonevu na upendeleo vikitawala. Ndiyo maana kwa sehemu somo linauliza, simba ataunguruma pasipo mawindo? Yaani simba akikosa chakula ataunguruma? Ndege atanaswa pasipo mtego? Maswali yanayoulizwa yanaonesha kwamba pasipo haki ni maumivu.

Ukisoma mbele unaona Bwana akitangaza adhabu kwa wote wasiotenda haki;

Amosi 3:10

Kwa maana hawajui kutenda haki, asema Bwana, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.

Pasipo haki hakuna utukufu wa Mungu, Yesu hawezi kudhihirika hapo. Tukitenda haki kila mmoja kwa nafasi yake Yesu anadhihirika pasipo shaka, maana yeye hutenda haki. Ni wito wangu kwako kutenda haki hapo ulipo, maana hilo ni agizo. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa