Date: 
14-01-2026
Reading: 
Warumi 2:11-13

Hii ni Epifania 

Jumatano asubuhi tarehe 14.01.2026

Warumi 2:11-13

11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.

13 Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.

Ubatizo wetu;

Msingi wa somo la leo asubuhi ni hukumu ya Mungu yenye haki. Katika kuliona hilo, Mtume Paulo anawaandikia Warumi kwamba kwa Mungu hakuna upendeleo. Yaani hapa Paulo alikuwa anawaambia kuwa mbele za Mungu haki hutawala, sheria hufuatwa zilivyo. Paulo anakazia kwamba watendao sheria ndiyo watakaohesabiwa haki.

Paulo anapoandika juu ya kufuata sheria, haki na hukumu hamaanishi kuifuata sheria kama ilivyokuwa Agano la kale, bali kuifuata Injili kwa kumwamini Yesu. Anawataka kuhamisha mawazo yao kutoka sheria ya Musa, kuwa kwa mtazamo wa Injili ya Yesu Kristo. Kwa maana hiyo, Paulo anasema wamwaminio Yesu ndiyo wataurithi uzima wa milele. Basi tudumu kwa Kristo tuliyempokea tulipobatizwa ili atupe mwisho mwema. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa 

Mlutheri