Date:
12-01-2026
Reading:
Warumi 6:3-4
Hii ni Epifania
Jumatatu asubuhi tarehe 12.01.2026
Warumi 6:3-4
3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Ubatizo wetu;
Juma hili tunatafakari juu ya ubatizo wetu, ambapo asubuhi hii tunamsoma Paulo akiwaandikia Warumi kwa kuwauliza, kwamba "hamfahamu ya kuwa sisi tuliobatizwa katika Kristo tulibatizwa katika mauti yake?" Paulo anaendelea kuandika kwamba kwa njia ya ubatizo tulizikwa na Kristo, kusudi kama Yesu alivyofufuka nasi tuenende katika upya wa uzima.
Paulo alikuwa anawaambia watu wa Kanisa la Korintho, kwamba kwa njia ya ubatizo walikufa na kufufuka na Kristo. Hapa Paulo alikuwa anawafundisha kuwa ubatizo waliobatizwa ulitoka kwa Kristo mwenyewe, na kwa njia ya ubatizo walikuwa na nafasi ya kuenenda katika uzima. Kumbe kwa njia ya ubatizo tunaye Yesu Kristo, basi nasi tuenende katika upya wa uzima. Amina
Uwe na wiki njema
Heri Buberwa
Mlutheri
