Date: 
09-01-2026
Reading: 
Kutoka 3:11-14

Hii ni Epifania 

Ijumaa asubuhi tarehe 09.01.2026

Kutoka 3:11-14

11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?

12 Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini?

14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Yesu ni nuru ya Ulimwengu;

Tunamsoma Musa akitumwa na Mungu kwenda kwa Farao kuwatoa wana wa Israeli, tayari kuianza safari ya kuiendea nchi ya ahadi. Musa anamuuliza Mungu kwamba yeye (Musa) ni nani hata aende kwa Farao kuwatoa Israeli Misri? Lakini Mungu anampa ahadi ya kuwa naye, na Israeli wote. Bado Musa anauliza akifika kwa Israeli aseme katuma na nani? Anaambiwa aseme ametumwa na MIMI NIKO AMBAYE NIKO

Huu ulikuwa ni mwanzo kwa wana wa Israeli kutoka Misri. Mpango wa Mungu kuokoa watu wake ulikuwa unaendelea, na ulitimia kwa Israeli kuondoka Misri kuelekea Kanani. Mpango huu wa ukombozi uliendelea kwa Mungu kuja kwetu kwa njia ya mwili, yaani Yesu Kristo, akafa na kufufuka kwa ajili yetu. Huyu Yesu ndiye nuru ambaye hutuangazia tutoke dhambini, na kutupa uzima wa milele. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri