Date: 
03-01-2026
Reading: 
Yeremia 46:27-28

Jumamosi asubuhi tarehe 03.01.2026

Yeremia 46:27-28

[27] Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
[28] Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

Uso wa Bwana uende pamoja nasi;

Somo la asubuhi hii ni ujumbe wa Bwana kwa Taifa lake kupitia kwa Nabii Yeremia kwamba wasiogope, maana yeye angewakomboa toka uhamishoni. Wanapewa ahadi ya kustarehe. Bwana anazidi kusisitiza kwamba yuko pamoja nao, lakini anawakumbusha kwamba atarudi kwa hukumu, hatawaacha bila adhabu.

Ni ahadi ya Bwana juu ya watu wake ambayo ilitimia maana Bwana hakuwahi kuwaacha. Anawatajia hukumu akiwataka kutenda yawapasayo ili wasiingie hukumuni. Ujumbe huu unatujia sisi leo asubuhi, kwamba Bwana yuko nasi katika mwaka huu. Anatukumbusha kutimiza wajibu wetu, maana kila mmoja atatoa hesabu ya uwakili wake. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya