Date: 
29-12-2025
Reading: 
1 Samweli 2:18-21

Hii ni Noeli;

Jumatatu asubuhi tarehe 29.12.2025

1 Samweli 2:18-21

18 Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za Bwana, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani.

19 Tena mamaye humfanyizia kanzu ndogo, na kumletea mwaka kwa mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka.

20 Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, Bwana na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa Bwana. Kisha wakaenda nyumbani kwao.

21 Naye Bwana akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za Bwana.

Mungu anatimiza ahadi zake;

Mtu mmoja aliyeitwa Elkana alikuwa na wake wawili, Hana na Penina. Penina alikuwa na watoto, Hana hakuwa na watoto. Hana aliishi maisha ya kukosa raha maana Penina alimringia sana mwenzake kwa kukosa watoto. Hana alipeleka kilio chake mbele za Mungu akiomba mtoto. Alitoa ahadi kwamba akipata mtoto atamtoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu. Mungu akamkumbuka Hana, akabeba mimba na kupata mtoto, ndiye Samweli.

Somo la asubuhi hii linamuonesha tayari Samweli akitumika mbele za Bwana. Mstari wa mwisho unaonesha Hana akizaa watoto wengine zaidi. Mungu alimpa Hana hitaji la moyo wake. Nasi tukimtazama Bwana anatimiza haja za mioyo yetu, maana ni ahadi yake kuwa nasi daima. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

Butainamwa, Bukoba